Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM ameanza ziara ya mataifa matano ya Afrika

KM ameanza ziara ya mataifa matano ya Afrika

KM wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliwasili Afrika Kusini siku ya Jumanne kuanza ziara yake ya nchi tano za Afrika, itakayomfikisha Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Misri.

Masuala muhimi yatakayo jadiliwa wakati wa ziaya yake yatakua juu ya amani na usalam, mabadiliko ya hali ya hewa na utawala bora, pamoja na mkutano wa kazi za kuikarabati Gaza huko Misri, kituo cha mwisho cha ziara yake. Akiwa huko Afrika kusini atakutana na viongozi wa serekali na viongozi wengine kama marais wa zamani Nelson Mandela, na Thabo Mbeki. Atazungumzia juu ya jukumu la nchi hiyo katika kuleta amani na usalama barani Afrika na juhudi zake za kuleta mabadiliko huko Zimbabwe. KM ataelekea Tanzania ambako kuna mpango wa majaribiyo kuratibu juhudi zote za UM katika kanda moja. Nchini DRC bw Ban atakutana na Rais Joseph Kabila na maafisa wa UM na kuwatembelea walinda amani wa UM huko Goma, na wathiriwa wa ubakaji na ghasia dhidi ya wanawake mjini Bukavu, katika hospitali ya Panzi. KM atakutana na Rais Paul Kagame wa Rwanda mjini Kigali. Na hatimae ataelekea Sharm el-Sheikh Misri kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa kusaidia uchumi wa Palestina kwa ajili ya kuikarabati Gaza.