Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM alaani vikali mauwaji ya walinda amani wa Umoja wa Afrika

KM alaani vikali mauwaji ya walinda amani wa Umoja wa Afrika

KM wa UM Ban Ki-moon alilaani vikali jana shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Afrika AU huko Mogadishu mji mkuu wa Somalia, lililosabibisha vifo vya walinda amani 11 wa Burundi.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji mwake amesema hapawezi kuwepo na sababu yeyote ya haki kwa shambulio hilo au mashambulio mengine ya karibuni dhidi ya vikosi vya AU walopelekwa kwa lengo pekee la kuwasaidia wananchi wa Somalia kuleta amani na usalama katika nchi yao.

Bw Ban alieleza masikitiko yake kutokana na vifo vilivyotokea na kueleza uungaji mkono wake wa dhati kwa AU na serekali ya Burundi iliyonesha uwongozi thabiti huko Somalia. Kumekuwepo na maendeleo ya kutia moyo mnamo mwezi uliyopita huko Somalia ambayo haijawahi kua na serekali kuu inyaofanywa kazi tangu 1991, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa rais mpya Sharif Sheikh Ahmed.