Skip to main content

Hapa na pale

Hapa na pale

Mjumbe maalum wa UM huko Somalia amesema alishutshwa na habari za shambulio dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Afrika huko Mogadishu, siku ya jumapili lililosababisha vifo vya wanajeshi 11 wa Burundi.

Bw Ahmedou Ould-Abdallah, anasema  anahakika shambulio lilifanywa  ili kubadilisha maoni kutokana na maendeleo mazuri yaliyopatikana hivi karibuni huko Somalia.

Naibu KM kwa ajili ya masuala ya uchumi na jamii Sha Zukang aliuambia mkutano wa UM kwamba changamoto kadhaa kuanzia mzozo wa chakula na fedha hadi mabadiliko ya hali ya hewa yanatishia juhudi za dunia kufikia maendeleo ya kudumu, au kukidhi mahitaji ya wakati huu bila ya kuhujumu uwezo wa vizazi vijao na mahitaji yao.