Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Qatar yatoa $ milioni 40 kwa ajili ya misaada ya dharura

Qatar yatoa $ milioni 40 kwa ajili ya misaada ya dharura

Serekali ya Qatar imetangaza hii leo kwamba imetoa msaada wa dola milioni 40 ili kusaidia mipango ya huduma za dharura ya UM kote duniani.

Dola milioni 30 imeahidiwa kwa ajili ya huduma za dharura huko Gaza na dola milioni 10 kupewa fuko la kujibu dharura CERF. Msaada huo unaifanya Qatar kua mfadhili mkuu wa tisa wa fuko hilo kwa mwaka 2009. Mratibu wa huduma za dharura za UM Bw John Holmes amesema huu ni msaada karimu na unakaribishwa sana kwa huduma muhimu za umoja huo kwa wakati huu.