Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu itatangaza uwamuzi wa kukamatwa au la kwa Rais wa Sudan hivi karibuni

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu itatangaza uwamuzi wa kukamatwa au la kwa Rais wa Sudan hivi karibuni

Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitangaza Jumatatu kwamba itatoa uwamuzi wake kuhusu kutowa kibali cha kukamatwa Rais Omar al Bashir wa Sudan hapo march 4, 2009.

Kufuatana na taarifa iliyotolewa huko The Hague, mahakimu watatoa uwamuzi wao kufuatana na maombi ya mwendesha mashtaka mkuu yaliyofikishwa July 14 mwaka jana ya kutaka kumfungulia mashtaka kiongozi huyo wa Sudan kwa uhalifu wa vita, mauwaji ya kimbari na mateso huko Darfur. Mapema mwezi huu baadhi ya maafisa wa UM na Marekanin walisema kwamba mahakimu wameshafikia uwamuzi wao na huwenda wakatangaza hivi karibuni, lakini ICC ilikanusha habari hizo.