Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walimaji wadogo wadogo wa Tanzania wapatiwa mkopo na UM

Walimaji wadogo wadogo wa Tanzania wapatiwa mkopo na UM

Walimaji wa mashamba madogo madogo huko Tanzania watafaidika kutokana na mkopo wa dola milioni 56 unaopatiwa sekta ya kilimo ya serekali kutoka UM.

Walimaji wa mashamba madogo madogo huko Tanzania watafaidika kutokana na mkopo wa dola milioni 56 unaopatiwa sekta ya kilimo ya serekali kutoka UM. Msaada huo wa ziada kutoka Idara ya Kiamtaifa ya Maendeleo ya Kilimo, IFAD itawasaidia wakulima wadiogo wadogo katika juhudi za kuhamasisha ukuwaji wa uchumi na kupunguza umaskini. Katika taarifa yake IFAD imeeleza kupanua masoko ya ndani na ya njee pamoja na idadi kubwa ya ardhi ya kulimwa Tanzania imetoa nafasi kwa wakulima kufaidika na kupanuka kwa mahiaji ya mazao ya kusafirishwa njee. Mkopo huo utatumiwa katika mradi wa kuwasaidia wanawake na wanaume maskini wa mashambani wanaoishi kwa chini ya dola moja kwa siku kuimarisha uzalishaji wao wa kilimo na mapato. Mradi wote unakadiriwa kugharibu zaidi ya dola milioni 315 katika kipindi cha miaka saba, ambapo wafadhili wakuu ni IFAD, Benki Kuu ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na Japan, Ireland na Umoja wa Ulaya.