Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNMIS asikitishwa na kifo cha mwandishi wa Sudan

Mkuu wa UNMIS asikitishwa na kifo cha mwandishi wa Sudan

Ashraf Jehangir Khan, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Sudan, ambaye pia ni Mkuu wa Shirika la UM juu ya Amani Sudan Kusini (UNMIS) amenakiliwa, kwenye taarifa kwa waandishi habari, kusikitishwa sana na kifo cha mwandishi mashuhuri wa riwaya wa Sudan, Al-Tayeb Saleh kilichotukia wiki hii.

 Kwa mujibu wa taarifa ya Khan, marehemu "atakumbukwa zaidi nchini Sudan, na pia katika mataifa mengine duniani, kwa umahiri wa kuandika fasihi ya masimulizi ya kubuni, iliokuwa na uwezo wa kuchanganua vyanzo vya utulivu kwenye mazingira ya tamaduni mbalimbali, yenye vizazi na umma tofauti ambao wote huishi pamoja kwa amani bila fujo." Kwa niaba ya UNMIS, Mjumbe wa KM aliitumia aila ya mwandishi Saleh, mkono wa taazia na pia kutoa pole kwa umma wa Sudan, marafiki wa marehemu na wale wanaopenda riwaya zake.