Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO inaadhimisha Siku ya Haki kwa Jamii Duniani

ILO inaadhimisha Siku ya Haki kwa Jamii Duniani

Ijumaa ya tarehe 20 Februari itaadhimishwa rasmi, kwa mara ya kwanza na Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) kuwa ni Siku ya Haki katika Jamii Duniani.

Mnamo Novemba 2007, Baraza Kuu la UM lilipitisha azimio liliopendekeza tarehe 20 Februari, kila mwaka, ihishimiwe kuwa ni Siku ya Haki katika Jamii Duniani. Shirika la ILO, kuiadhimisha siku hiyo kwa mwaka huu, limeandaa warsha maalumu utakaojadilia mada inayouliza kama "Mzozo wa kimataifa: ni tishio au fursa ya kuimarisha haki kwa umma?." Warsha wa ILO, utafanyika mjini Geneva, na utakusanyisha wawakilishi kutoka vyuo vikuu, sekta ya fedha, mashirika ya kimataifa, mashirika yasio ya kiserikali na kutoka ulimwengu wa ajira, ambapo wajumbe wanatarajiwa kubadilishana mawazo juu ya sera za kuchukuliwa kukabiliana na mizozo iliopamba ulimwenguni sasa hivi, yaani ile migogoro inayoambatana na mazingira dhaifu, uchumi ulioregarega na matatizo ya chakula; na pia kusailia athari zake kwenye zile huduma za kutekeleza haki katika jamii.