Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP imepongeza Olimpiki ya Beijing kwa kutekeleza miradi ya Mazingira Rafiki

UNEP imepongeza Olimpiki ya Beijing kwa kutekeleza miradi ya Mazingira Rafiki

Baraza la Utawala la Shirika la UM Juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limewasilisha matokeo ya ripoti maalumu ya utafiti wao, kuhusu utekelezaji wa huduma za kimazingira wakati wa mashindano ya Olimpiki ya Beijing.

Ripoti ilisema waandalizi wa mashindano ya Olimpiki ya Beijing ya 2008 walifanikiwa kutekeleza, kwa kiwango kilichovuka mapendekezo ya kuhifadhi mazingira ya Shirika la UNEP - mathalan, hewa chafi inayomwagwa angani ilipunguzwa kwa kima kikubwa kabisa kwenye mji wa Beijing wakati wa mashindano ya Olimpiki; na Serikali, vile vile iliwekeza posho kubwa ya fedha katika kuimarisha usafiri wa umma, wa hali ya juu, na mashindano yalifanyika kwa hali ilioonyesha hisia kubwa ya kuihifadhi mazingira. Lakini ripoti ya UNEP pia ilisema ingelipendelea kuona mashirika yasio ya kiserikali yakishirikishwa zaidi kwenye Olimpiki ya Beijing ya 2008.