Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viwavi haribifu vinahatarisha kilimo Liberia, imehadharisha FAO

Viwavi haribifu vinahatarisha kilimo Liberia, imehadharisha FAO

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) leo limewatangazia waandishi habari mjini Monrovia, kwamba taifa la Liberia limevamiwa na aina ya viwavi visiojulikana, na wakati huo huo vile viwavi vinavyohujumu mimea, vimegundulikana kuvuka mipaka na kuelekea taifa l Cote d\'Ivoire.

Waziri wa Kilimo wa Liberia, Christopher Toe alithibitisha taarifa hizo. Viwavi vipya visiojulikana vina rangi nyeupe na nyeusi, wakati wale viwavi walioshambulia mimea katika maeneo ya Bong, Gbarpolu, Nimba na Lofa, Liberia wana rangi nyeupe na manjanao. Viwavi viharibifu vilihujumu miti ya kahawa na kakao, mimea ambayo huzalisha mazao yenye natija kubwa ya kibiashara nchini.