Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kinga za Maradhi kwa Watoto zasailiwa kwenye mkutano ulioanza rasmi Makao Makuu

Kinga za Maradhi kwa Watoto zasailiwa kwenye mkutano ulioanza rasmi Makao Makuu

Washirika wa kwenye zile juhudi za kupiga vita maradhi yanayozuilika kwa chanjo, wamekusanyika kwenye Makao Makuu ya UM wiki hii, kuhudhuria kikao cha nne cha Mkutano wa Kukinga Maradhi Duniani.

Mkutano huu wa mwaka utachukua siku tatu na umetayarishwa na Shirika la Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF), Shirika la Afya Duniani (WHO) na Umoja wa GAVI. Mkutano utalenga majadiliano kuhusu maendeleo kwenye zile huduma za kuchanja watoto ulimwenguni. Kwa mujibu wa Peter Salama, Mkuu wa Afya katika Shirika la UNICEF, "mkutano utawapatia wajumbe wa kimataifa fursa ya kufafanua hatua zilizofikiwa kimataifa kwa sasa, na miradi inayohitajika, kudhibiti bora juhudi muhimu za kuchanja watoto wadogo dhidi ya maradhi yanayozulika." Alisema maisha ya watoto milioni 2 ziada yatahifadhika, kila mwaka, hasa katika kuwakinga na "homa ya vichomi na maradhi ya kuharisha, magonjwa ambayo ndio yenye kuongoza katika kusababisha vifo, kwa wingi, miongoni mwa watoto wachanga chini ya umri wa miaka mitano" pindi huduma za kuchanja watoto wadogo zitakithirishwa kimataifa. Kadhalika, mpango unaojulikana kama Mradi wa GIVS, yaani Mradi wa Kukinga Maradhi Duniani, uliobuniwa shirika na UNICEF na WHO, utazingatiwa kwa kiwango cha hadhi ya juu na wajumbe wa kimataifa. Lengo la Mradi wa GIVS ni kuhakikisha angalau asilimia 90 ya watoto wanaohitajia kuchanjwa dhidi ya maradhi yanayozuilika watapatiwa tiba hiyo katika kila taifa itakapotimu 2010.