Mkuu wa UNESCO alaani vifo vya waandishi habari katika JKK na Bukini

17 Februari 2009

Koichiro Matsuura, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) amelaani mauaji ya waandishi habari yaliotukia majuzi katika Jamhuri ya Kongo na Bukini.

Bruno Ossébi, aliyekuwa na umri wa miaka 43, na akiandikia gazeti linaloitwa Mwinda, alifariki kwenye hospitali ya kijeshi mjini Brazzaville, baada ya kupata mejeraha, kufuatia kuchomwa moto nyumba yake, mwisho wa mwezi Januari. Umaarufu wa Ossébi ulikuwa katika kufichua ulajirushwa wa hadhi ya juu uliokuwa ukifanyika nchini mwao. Matsuura aliwaomba wenye madaraka kuhakikisha waliosababisha kifo cha mwandishi habari Ossébi watashikwa na kufikishwa mahakamani. Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, vile vile alishtumu mauaji ya Ando Ratovonirana, aliyekuwa na umri wa miaka 25, mwandishi habari wa Radio et Télévision Analamanga (RTA), ambaye aliuawa kwenye mji wa Antananarivo, mnamo Februari 7, wakati alipokuwa akiripoti maandamano ya kupinga serikali nje ya nyumba ya raisi. Matsuura aliwaomba wenye madaraka kuhakikisha usalama wa waandishi habari nchi, hata wakati wa fujo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter