Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mshindi wa Tunzo ya Haki za Binadamu, kutokea JKK, azungumzia uokoaji afya ya wasibiwa na uhalifu wa nguvu wa kijinsia

Mshindi wa Tunzo ya Haki za Binadamu, kutokea JKK, azungumzia uokoaji afya ya wasibiwa na uhalifu wa nguvu wa kijinsia

Makala yetu maalumu, kwa leo, itazingatia juhudi za daktari mmoja shujaa, kutokea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), aliyehamasishwa kiutu na kizalendo, kujishirikisha kwenye huduma za kufufua afya ya wale wanawake, na watoto wa kike, waliosibiwa na mateso ya jinai ya kunajisiwa kimabavu na kihorera, kutokana na mazingira ya vurugu kwenye eneo la mashariki ya JKK.

Wiki iliopita, Dkt Denis Mukwege, Mkurugenzi wa Hospitali ya Panzi, iliopo Bukavu katika JKK alizuru Makao Makuu ya UM.  Mwaka jana Dktr Mukwege altunukiwa Tunzo ya UM ya Mtetezi Jasiri wa Haki za Binadamu, kwa mchango wake muhimu katika huduma za kusaidia kurudisha afya bora, kwa wale wanawake waliokamatwa kwa nguvu na kunajisiwa kihorera na wanaume wafuasi wa makundi mbalimbali yanayochukua silaha, yanayohasimiana nchini humo.  Alipokuwepo New York, nilipata fursa ya kumfanyia mahojiano Dktr Mukwege ambaye alituelezea mchango namna anavyojitahidi kukabiliana na tatizo sugu la madhila ya kijinsiya, tatizo ambalo bado linaendelea kusumbua umma wa eneo. Alibashiria hatua alizopendelea UM kujihusisha nazo kukomesha, halan, karaha ovu ya kunajisi wanawake kihorera na kuwaharibu njia zao za kufanyika haja. 

   Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.