Mradi wa vocha za chakula waanzishwa Burkina Faso na WFP

13 Februari 2009

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeanzisha mradi wa kutoa vocha, au hati kwa watu wenye kufadhiliwa chakula katika mataifa ya Afrika, hasa kwa wale wakazi wa katika miji.

Utaratibu huu utatumiwa kurahisisha operesheni za WFP za kugawa chakula, kwa umma muhitaji wa miji, ambapo licha ya kuwa chakula huwa kinapatikana lakini kwa sababu ya bei kubwa ya vyakula kutokana na matatizo katika soko la kimataifa, UM umelazimika kurekibisha utaratibu unaotumia kugawa chakula katika mataifa yenye shida,na kuusaidia umma husika. Operesheni ya kwanza itaanzishwa katika mji wa Ouagadougou, Burkina Faso kuhudumia watu 120,000 ambao wanakabiliana na tatizo la kuongezeka kwa bei za chakula kikuu cha umma, kama mtama, kwa asilimia 25, bei ambayo watu wa kawaida hawaimudu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud