Uzalishaji wa nafaka unaashiriwa na FAO kuporomoka kwa mwaka huu

12 Februari 2009

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limewakilisha ripoti inayozingatia hali ya uzalishaji wa nafaka, kwa mwaka huu, katika dunia.

Ripoti inahadharisha kwamba kutokana na hali ya hewa mbaya iliotanda kimataifa, ikichanganyika na mizozo yenye vurugu kali na bei za kigeugeu kwenye soko la kimataifa, kunaashiriwa uzalishaji wa mazao ya nafaka katika dunia utaporomoka, kwa kiwango kikubwa kabisa, katika mazingira ambayo watu bilioni 1 huteswa na matatizo ya njaa. Kuhusu ukanda wa Afrika Mashariki, ripoti inasema watu milioni 18 ziada wanakabiliwa na tatizo la chakula kieneo kwa sababu ya migogoro isiokwisha, machafuko, hali ya hewa mbaya au mchanganyiko wa vipengele hivyo, na wakati huo huo hali Kusini mwa Afrika inaonyesha watu milioni 8.7 wanakabiliwa, kila kukicha, na matatizo yanayotokana na usumbufu wa njaa na chakula, na hali ni mbaya zaidi, ilitilia mkazo FAO, katika mataifa ya Kenya, Usomali na Zimbabwe.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter