Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNODC imewakilisha ripoti mpya kuhusu biashara ya magendo ya kuchuuza watu wanaotoroshwa

UNODC imewakilisha ripoti mpya kuhusu biashara ya magendo ya kuchuuza watu wanaotoroshwa

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) limewasilisha "Ripoti ya Dunia juu ya Utoroshaji Magendo wa Watu kwa 2007 - 2008".

Takwimu zilizokusanywa katika kipindi hicho zinawakilisha ushahidi kutoka nchi 155, unaoeleza, kwa kina, kiwango cha biashara haramu ya magendo ya kutorosha watu wanaolazimishwa kushiriki kwenye kadhia zilizo nje ya sheria, mathalan, umalaya, askari watoto, au watoto wa kupanga waliochukuliwa kinyume cha sheria. Vile vile ripoti inasailia tatizo la uhamishaji haramu wa viungo vya wanadamu ili kupata faida. Kadhalika, ripoti inafafanua na kupendekeza aina ya hatua za kuchukuliwa kisheria na Mataifa Wanachama, ili kukabiliana bora na matatizo haya ya jinai, na pia kuelezea mwelekeo halisi juu ya vitendo vya kutorosha watu ulimwenguni.