Wahamiaji 25,000 wa JKK katika Zambia waiomba UM iwarejeshe makwao

Wahamiaji 25,000 wa JKK katika Zambia waiomba UM iwarejeshe makwao

Shirika la UM Juu ya Wahamiaji (UNHCR) limeripoti asilimia 99 ya wazalendo wahamiaji 25,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), waliopo kwenye kambi za Kala na Mwanga, nchini Zambia wameomba warejeshwe makwao na UM. Kambi hizi mbili zipo katika eneo la Zambia kaskazini, kilomita 1,000 kutoka mji mkuu wa Lusaka.

Serikali ya Zambia, ikishirikiana na UNHCR zimo mbioni kukithirisha kampeni ya kueneza taarifa za kuwasaidia wahamiaji husika kujiyatarisha na kujua hali halisi ilivyo makwao, kabla hawajarejeshwa huko kwa hiyari.