Mahakama ya ICC inakana tetesi za kufikia uamuzi wa kumshika Raisi wa Sudan

Mahakama ya ICC inakana tetesi za kufikia uamuzi wa kumshika Raisi wa Sudan

Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) imetangaza taarifa maalumu, inayokana zile tetesi zilizosambaa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, zinazodai kwamba mahakimu wake wamefikia uamuzi wa kutoa hati ya kumshika Raisi Omar Al Bashir wa Sudan.

Taarifa inasisitiza majaji wa Mahakama Ndogo ya ICC, Inaozingatia Ukweli na Sheria juu ya madai ya Mwendesha Mashitaka, kabla ya kesi, hawakuidhinisha waraka wa aina yoyote dhidi ya Raisi wa Sudan, kuambatana na ombi la Mwendesha Mashitaka la Julai 14, 2008.