Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi wa bunge la Usomali wapongezwa na UM

Uchaguzi wa bunge la Usomali wapongezwa na UM

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould Abdallah mapema wiki hii ametoa taarifa yenye kusifu namna uchaguzi wa kuteua wabunge wa Usomali ulivyoendeshwa karibuni nchini Djibouti, uchaguzi ambao alisema ulihudumiwa “kwa uwazi na bila kificho.”