Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF inaomba ifadhiliwe dola milioni 34 kuhudumia waathirika wa mashambulio na uvamizi katika Ghaza

UNICEF inaomba ifadhiliwe dola milioni 34 kuhudumia waathirika wa mashambulio na uvamizi katika Ghaza

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Mendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetoa ombi liliopendekeza lifadhiliwe haraka mchango wa dharura wa kukidhi mahitaji ya kihali, kwa wale watoto na aila zao, ambao waliathirika hivi majuzi kutokana na mashambulio ya mabomu na vurugu lilioendelezwa na vikosi vya Israel kwenye Tarafa ya Ghaza.

UNICEF inaomba ifadhiliwe msaada wa dola milioni 34 ziada,fedha ambazo zikipokewa, zitaiwezesha UNICEF kuhudumia karibu miradi 20 muhimu, kwa makusudio ya kuwapatia watoto hifadhi kinga, huduma za afya, lishe bora, maji safi na salama pamoja na kuwapatia mazingira safi, elimusiha na vile vile kuimarisha vizuri zaidi sekta ya elimu. Fungu kubwa la msaada unaotakiwa na UNICEF kwa sasa, unaokadiriwa dola milioni 12, litatumiwa kwenye ile miradi ya kuwapatia watoto ulinzi bora kwenye mazingira ya hali ya hatari; na vile vile kunahitajika dola milioni 9.4 ziada kuwatekelezea watoto mahitaji yao kwenye sekta ya elimu.