UNHCR/Kenya wakagua maskani mapya kwa wahamiaji wa Usomali
Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti Serikali ya Kenya imekubali kutenga ardhi maalumu, katika eneo la kaskazini mashariki ya nchi, ili kuwaweka wahamiaji wa Usomali, wanaomiminikia Kenya sasa hivi kwa idadi kubwa.