Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake lazima washirikishwe kwenye maamuzi ya migogoro ya uchumi, imenasihi CEDAW

Wanawake lazima washirikishwe kwenye maamuzi ya migogoro ya uchumi, imenasihi CEDAW

Kamati ya UM ya Kuondosha Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW) juzi imewasilisha taarifa maalumu kutoka Geneva, inayozihimiza Serikali Wanachama kuwahusisha wanawake kwenye maamuzi ya kutatua mizozo ya kiuchumi iliokabili ulimwenngu kwa sasa hivi, mizozo ambayo athari zake ndizo zenye kuzorotisha mipango ya maendeleo ya kukamilisha usawa wa kijinsiya kimataifa.