Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naibu KM wa masuala ya kiutu akutana na waathirika wa vurugu Kivu Kaskazini

Naibu KM wa masuala ya kiutu akutana na waathirika wa vurugu Kivu Kaskazini

Naibu KM wa Masuala ya Kiutu, John Holmes, Ijumapili alizuru jimbo la mgogoro la mashariki, katika JKK, ambapo alipata fursa ya kujionea, binafsi, athari za kimwili na kiakili walizopata raia wa kiume, wanawake pamoja na watoto, alipotembelea hospitali ya Heal Africa, iliopo Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.