Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Helikopta ya UNAMID yashambuliwa risasi Darfur

Helikopta ya UNAMID yashambuliwa risasi Darfur

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) limeripoti kwamba mnamo Ijumatatu, helikopta yao ya aina ya Mi-8, ilishambuliwa kwa risasi na washambulizi wasiojulikana, kwenye eneo liliopo kilomita 70 kusini magharibi ya mji wa El Fasher, wakati helikopta hiyo ilipokuwa inapeleka vyakula kwa walinzi wa amani.