Raia wa JKK wamiminikia Sudan Kusini kukwepa ukatili wa LRA, imeripoti UNHCR
Ron Redmond, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) amenakiliwa na waandishi habari wa kimataifa waliopo katika Ofisi ya UM Geneva akisema kwamba waasi wa Uganda wa kundi la LRA walishambulia tena wiki iliopita maeneo ya JKK na kusababisha maelfu ya raia kukimbilia taifa jirani la Sudan Kusini:~