Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

BU na KM wasailia hali baada ya kuingia Ghaza kwa majeshi ya Israel

BU na KM wasailia hali baada ya kuingia Ghaza kwa majeshi ya Israel

KM Ban Ki-moon, kwenye taarifa iliotolewa na msemaji wake, alinakiliwa akisema ameingiwa na “wasiwasi mkubbwa kuhusu athari mbaya kufuatia kuanzishwa kwa operesheni za ardhini za vikosi vya Israel katika Tarafa ya Ghaza” Ijumamosi (03/01/2009), wakati ambao Baraza la Usalama (BU) vile vile liliamua kuitisha kikao cha dharura kuzingatia hali hiyo ya uhasama Ghaza.

KM alisisitiza, na kutilia mkazo kwenye risala yake, kwamba vurugu liliojiri Ghaza leo hii “litazusha vizingiti vipya, kadhaa, dhidi ya zile juhudi za kundi la wapatanishi wa kimataifa wa pande nne – yaani Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Urusi na Marekani na wadau wengineo – za kuleta amani katika eneo hilo la Mashariki ya Kati. Alirudia tena ombi la kutaka mapigano yakomeshwe haraka, na vile vile kuyahimiza “mashirika wenzi ya kimataifa, na kikanda, kutumia uwezo wote walionao, kukomesha umwagaji wa damu uliopamba sasa hivi na kusitisha mateso dhidi ya raia” wa eneo la vurugu.