Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Kwenye mkutano wa hadhara, asubuhi, na watumishi wa UM, KM Ban Ki-moon alisema mgogoro uliopamba sasa hivi katika Tarafa ya Ghaza, na pia Israel kusini, umesasbabisha uharibifu zaidi katika saa 48 zilizopita. Alisema mateso na maumivu yaliowakumba raia yanashtusha, na alisisitiza operesheni za vikosi vya Israel zilizoanzishwa Ijumamosi ndani ya Ghaza yenyewe, zimeharibu kabisa hali katika eneo hilo.~

KM ametuma risala ya pongezi kwa umma na Serikali ya Ghana, kwa kufanikiwa kukamilisha duru ya pili ya uchaguzi wa uraisi na bunge bila ya fujo. Kamisheni ya Taifa ya Uchaguzi katika Ghaza iliripotiwa iliongoza uchaguzi kwa umahiri mkubwa. Risala ya KM pia imevipongeza vyama vya kisiasa kwa kushiriki kwenye uchaguzi kwa amani.