Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suluhu ya mzozo wa Ghaza ipo na UM, asisitiza KM

Suluhu ya mzozo wa Ghaza ipo na UM, asisitiza KM

Imetangazwa asubuhi ya leo kwamba KM Ban Ki-moon atakutana, Ijumanne, na mawaziri wa nchi za kigeni wa kutoka mataifa ya KiArabu, pamoja na wadau wengine muhimu, ili kutathminia taratibu za pamoja za kuhamasisha Baraza la Usalama kuchukua hatua za haraka ili kusitisha mapigano katika Ghaza, na kuiwezesha jumuiya ya kimataifa kuhudumia vizuri zaidi misaada ya kiutu, kwa

KM, kwa upande wake, amemtaka Robert Serry, Mratibu Maalumu wa UM juu ya Mpango wa Amani kwa Mashariki ya Kati, arejee New York kutokea Israel, ili kumshauri juu ya hali halisi ilivyo katika Tarafa ya Ghaza, na pia kumsaidia KM kufafanua kihakika juhudi za kisiasa zinazoendelezwa kieneo ili kukomesha mapigano.

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM kuhusu Huduma za Wahamiaji (UNHCR), ametoa taarifa yenye kukumbusha tena kwamba kanuni za kiutu za kimataifa ni lazima zihishimiwe na kutekelezewa waathirika wa vurugu la Ghaza, hasa miongoni mwa yale mataifa jirani na Ghaza, ambayo hutarajiwa kuruhusu raia wanaokimbia vurugu na mapigano kuingia nchini mwao, na kuwapatia hifadhi ya kisiasa na usalama.

Kadhalika, asubuhi ya leo, wajumbe wa Kamati ya Mawaziri wa KiArabu wa Nchi za Kigeni juu ya Falastina wanakutana Makao Makuu kwa mashauriano juu ya matayarisho ya kikao kijacho cha Baraza la Usalama, kinachotarajiwa kukutana Ijumanne ya kesho.