UNRWA yahadharisha 'hali mbaya ya Ghaza lazima idhibitiwe haraka kunusuru maisha ya umma'

6 Januari 2009

Shirika la UNRWA linasema kuna dharura ya kusimamisha mapigano na vurugu katika Ghaza, haraka iwezekanavyo, ili kuhakikisha kunapatikana angalau upenu utakaoruhusu misaada ya kiutu, ya dharura, kuingizwa kwenye eneo la mtafaruku na kunusuru maisha ya umma waathirika, umma ambao sasa hivi hauana mahali pengine salama pa kukimbilia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud