Mashambulio ya Israel yaua darzeni za watu kwenye skuli za UM Ghaza

6 Januari 2009

Hii leo, vurugu la eneo liliokaliwa la WaFalastina, katika Tarafa ya Ghaza, limeingia siku ya 11 tangu vikosi vya Israel vilipoanzisha operesheni za kijeshi pamoja na mashambulio kwenye eneo hilo.

“Ripoti ya jeshi la Israel inadai kwamba wao ati hulenga ile miundombinu inayotumiwa na wapambanaji tu! Kama ni hivyo, kama madai hayo yana ukweli wo wote, tungependa kusema majengo ya UM yalioshambuliwa sasa hivi yanatumiwa kupokea raia wa Ghaza walion’golewa makwao. Majengo yetu yote haya – yakijumulisha pia skuli, vituo vya afya na vituo vya ugawaji misaada ya kiutu – yote yana plani ambazo zinajulikana vizuri na vikosi vya Israel, na ramani ya majengo yote ya UM hukabidhiwa wenye madaraka Israel kila wakati, ili kuhakikisha hakutofanyika makosa ya mashambulio na ndege za kivita, kutokea angani, na kujiepusha na ajali za ardhini, kama inavyofanyika mara kwa mara kutokana na uvamizi wa eneo liliokaliwa, la WaFalastina, la Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan.”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud