Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taasisi za Umoja wa Mataifa zinakutana kusailia mzozo wa Ghaza

Taasisi za Umoja wa Mataifa zinakutana kusailia mzozo wa Ghaza

Baraza la Usalama limekutana leo hii, kwa mara ya pili tena, kuanzia saa tano ili kuendelea na majadiliano ya hadhara juu ya mzozo wa kiutu uliolivaa eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza.

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu limeitisha kikao maalumu mjini Geneva Ijumaa ijayo, kuzingatia hali katika Tarafa ya Ghaza kufuatia ombi la kutoka mataifa ya KiIslam na nchi zinazoendelea, zikijumuika na taifa la Urusi vile vile.