Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA inasema hali Ghaza, kijumla, ni ya kushtusha kabisa

UNRWA inasema hali Ghaza, kijumla, ni ya kushtusha kabisa

Christopher Gunnes, Msemaji wa Shirika la UM Linalofarajia Wahamiaji wa KiFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA), ameiambia Redio ya UM-Geneva, kwamba hali katika Tarafa ya Ghaza ni mbaya sana, na kila saa masaibu na maafa ya kiutu yanaendelea kukithiri. Alisema watu milioni moja

“Ikiwa watu hawana imani na hali inayodaiwa kusimamisha mapigano, na huu ndio umma ambao, kwa muda wa karibu wiki mbili mfululizo, ulivumulia mashambulio ya mabomu, kutoka ndege za kijeshi, ikimaanisha saa tatu za kusisitishwa mashambulio haziwatoshi wao kuendeleza shughuli za kujihudumia kimaisha.” Alisema tunawajibika “kusikiliza ushauri na nasaha ya KM” .. inayopendekeza kudumisha usimamishaji wa mapigano katika Tarafa ya Ghaza, na sio kusitisha mashambulio kwa saa tatu tu. Alikumbusha, umma wa Ghaza umeshateseka kwa muda mrefu, na wakati umewadia kwa uhasama kukomeshwa, halan, na mizinga na bunduki za wanaohasimiana kunyamazishwa milele.