Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Kwenye barua aliotuma Kiyo Akasaka, Naibu KM juu ya Mawasiliano na Habari za Umma, kwa Mjumbe wa Kudumu wa Israel katika UM, amependekeza kwa Serikali ya Israel kuhakikisha waandishi habari wa kimataifa huwa wanapatiwa, haraka iwekanavyo, vibali vya kuingia kwenye Tarafa ya Ghaza kujionea wenyewe, na kuelezea hali halisi ilivyo kwenye mazingira yalioshuhudia mashambulio kadha ya ndege za kivita, manowari na vifaru vya vikosi vya Israel. Alikumbusha kwenye barua yake kwamba azimio nambari 1738 la Baraza la Usalama limesisitiza, wazi kabisa, ya kuwa makundi yote yanayohusikana mapigano yanawajibika kuhishimu uhuru na haki ya waandishi habari kuendeleza kazi zao, bila pingamizi, kwenye eneo la uhasama.

Kemal Dervis, Mkuu wa Shirika la UM kuhusu Miradi ya Maendeleo (UNDP), amemwarifu KM nia ya kujiuzulu kazi kuanzia Machi 01, 2009, kwa sababu za binafsi na za kiaila. KM alisema ameridhia uamuzi wa Dervis, lakini kwamasikitiko makubwa. Alisema karibuni ataanzisha utaratibu wa kutafuta Ofisa mwengine wa kusimamia shughuli za ofisi ya UNDP iliopo Makao Makuu.

Majadiliano ya upatanishi baina ya Serikali ya JKK na wawakilishi wa kundi la waasi la CNDP bado yanaendelea mjini Nairobi kuzingatia uwezekano wa kurudisha tena utulivu, na amani, kwenye jimbo la magharibi la Kongo. Mpatanishi Mwenzi wa majadiliano hayo, Raisi mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa, aambayendiye mwenye kusimamia duru ya pili ya mazungumzo hayo, amenakiliwa akisema makundi husika na mzozo wa Kongo mashariki yanajadilia masuala muhimu, kwa tahadhari sana, na polepole kabisa. Mazungumzo yanatarajiwa kuendelea tena Ijumaa.