Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Haki za Binadamu lakutana Geneva kusailia ukiukaji dhidi ya raia Ghaza

Baraza la Haki za Binadamu lakutana Geneva kusailia ukiukaji dhidi ya raia Ghaza

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu limeitisha kikao maalumu leo Ijumaa, mjini Geneva, kuzingatia hali katika Tarafa ya Ghaza.

“Azimio la Baraza la Usalama liliopitishwa kusimamisha mapigano katika eneo la Ghaza, ni lazima litekelezwe, haraka, ili kuruhusu kupeleka misaada ya kihali ya kunusuru maisha, angalau kwa wastani, inayohitajika kidharura na waathirika raia katika Tarafa ya Ghaza, na kuwawezesha pia majeruhi kusaidiwa kupelekwa kwenye maeneo ili kupata matibabu. Ninasisitiza umuhimu wa kupeleka tume maalumu ya waangalizi wa UM, wanaosimamia utekelezaji wa haki za binadamu, katika Israel na kwenye Maeneo Yaliokaliwa ya WaFalastina (OPT), watakaothibitisha, kipekee, uharamishaji wa haki za binadamu pamoja na ukiukaji wa sheria za kiutu za kimataifa.”