Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yadai ahadi za kuaminika kutoka Israel kuhifadhi watumishi

UNRWA yadai ahadi za kuaminika kutoka Israel kuhifadhi watumishi

Shirika la UM Linalofarajia Huduma za Kiutu kwa Wahamiaji wa KiFalastina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA), limetoa taarifa maalumu kwa vyombo vya habari, Ijumaa, inayoeleza ya kuwa limelazimika kusitisha, kwa muda, operesheni zake za kugawa misaada ya kiutu katika Tarafa ya Ghaza kwa sababu ya ukosefu wa usalama wa wafanyakazi wake.