BU lapitisha azimio la kusimamisha mapigano Ghaza

BU lapitisha azimio la kusimamisha mapigano Ghaza

Alkhamisi usiku, Baraza la Usalama lilipitisha azimio nambari 1860 (2009), liliodhaminiwa na Uingereza, lenye mwito wa kutaka mapigano yasitishwe haraka katika Tarafa ya Ghaza, na makundi yote yanayohasimiana na kuruhusu misaada ya kiutu kufikishiwa umma waathirika, bila vizingiti, na papo hapo kupendekeza majeshi ya Israel yaondoshwe kikamilifu kutoka eneo hilo.