Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Kwenye mkutano wa, awali, wa mwaka na waandishi habari kwenye Makao Makuu ya UM, KM Ban Ki-moon aliwasilisha ujumbe maalumu kuhusu vurugu liliopamba eneo la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza, ujumbe ambao alisema ulio na lugha isio ngumu, ulio wazi na wa maana, wenye kuyanasihi makundi yenye kuhasimiana “kukomesha mapigano, haraka .. sasa hivi”. Alikumbusha kwamba watu wingi wameshafariki kutokana na uhasama huo katika Ghaza, hali ambayo imewafanya raia wa Israel na umma wa WaFalastina kujikuta wanaishi “maisha ya khofu” kila kukicha. Alisema mazingira ya Tarafa ya Ghaza, ndipo penye chimbuko na “msingi wa umma wa KiFalastina unaoshuhudia maangamizi: nyumba

Katika mwisho wa wiki iliopita, Shirika la Afya Duniani (WHO) limewakilisha ripoti mpya yenye kuonyesha hali halisi ya udhibiti wa mripuko wa maradhi ya kipindupindu Zimbabwe kwa sasa. Ripoi ilisema swagonjwa 38,000 walisajiliwa kuambukizwa na maradhi na watu 1,900 walishafariki kutokana na maradhi. Kwa mujibu wa WHO maradhi yamepamba kkatika nchi nzima, na kuathiri majimbo yote pamoja na asilimia 90 ya wilaya sitini na mbili.