Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

John Holmes, Mkuu wa Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) na Naibu KM kuhusu Masuala ya Kiutu ameidhinisha dola milioni saba kutoka Mfuko wa UM juu ya Maafa ya Dharura/Mfuko wa CERF, zitumiwe kidharura kuhudumia misaada ya kihali kwa umma ulionaswa kwenye mazingira ya mapigano katika Tarafa ya Ghaza.

Baraza la Usalama asubuhi lilipitisha maazimio mawili kuhusu masuala ya uslama na amani Afrika. Azimio la awali lilizingatia mzozo wa mipaka kati ya Djibouti na Eritrea, ambapo wajumbe wa Baraza waliyasihi mataifa haya mawili ya Pembe ya Afrika kujitahidi kusuluhisha siotafahamu zao kwa njia ya amani; na wakati huo huo kuitaka Ethiopia kuondosha vikosi vyake na vifaa vya kijeshi na kurejea kwenye eneo la kabla ya mzozo wao kufumka. Azimio la pili liliambatana na uamuzi wa Baraza la Usalama kuongeza muda wa kuwepo huduma kadha za kimataifa katika Chad, kwa kipindi cha mwaka mmoja, na wakati huo huo kuongeza muda wa operesheni za Shirika la UM la MINURCAT katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad hadi tarehe 15 Machi 2010. Baadaye Baraza la Usalama lilifanyisha majadiliano, kwenye kikao cha hadhara, kuzingatia hifadhi ya raia kwenye mazingira ya uhasama, ambapo wajumbe wa kimataifa 50 walihutubia.