Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO linatarajiwa kuanzisha uchanjaji wa homa ya manjano katika Guinea

WHO linatarajiwa kuanzisha uchanjaji wa homa ya manjano katika Guinea

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kwamba, litajihusisha na uchanjaji wa watu 60,500 dhidi ya homa ya manjano katika Guinea, kuanzia tarehe 26 Januari (2009) baada ya watu wawili kugundulikana waliambukizwa na maradhi haya maututi katika wilaya ya Faranah, iliopo katika Guinea ya kati, karibu na Mto Niger. Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na maabara ya kikanda ya Taasisi ya Pasteur, Dakar, Senegal hatua hii inachukuliwa mapema ili kudhibiti haraka ugonjwa usije ukaripuka na kuenea kwenye taifa hilo husika. ~