Mkuu wa UNICEF asisitiza watoto Ghaza lazima wahifadhiwe
Ann Veneman, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) ametoa taarifa maalumu yenye mwito unayoyataka makundi yanayohusika na mapigano yanayoendelea Ghaza, kuhakikisha watoto wanapatiwa hifadhi imara, dhidi ya mashambulio.