Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM aongeza jitihadi za kidiplomasiya kusitisha mapigano Ghaza

KM aongeza jitihadi za kidiplomasiya kusitisha mapigano Ghaza

Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la UM Linalofarajia Wahamiaji wa Mashariki ya Karibu (UNRWA) mapigano yamezidisha ukali katika Tarafa ya Ghaza baina ya majeshi ya Israel na wapiganaji wa KiFalastina.

“KM alikuwa na mazungumzo Cairo na Raisi [Hosni] Mubarak [wa Misri], Waziri wa Mambo ya Nje, Ahmed AboulGheit, na vile vile KM wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Amr Moussa; na alisisitiza kwenye mazungumzo yao kwamba dhamira hasa ya ziara yake ni kuhamasisha viongozi wa mataifa ya eneo, na hususan wale wahusika wakuu wawili [yaani Israel na wapiganaji wa KiFalastina], kutekeleza kikamilifu azimio 1860 (2009) la Baraza la Usalama, la kuhakikisha mapigano yanasitishwa haraka hivi sasa, ili kuruhusu misaada ya kihali na kiutu kuhudumiwa waathirika na umma muhitaji katika Ghaza, na pia kuruhusu juhudi za kujenga upya [mioundombinu ya kiuchumi na jamii ilioharibiwa na mapigano].”