Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Hivi sasa Ofisi ya Mratibu Maalumu wa UM kuhusu M[pango wa Amani kwa Mashariki ya Kati (UNSCO) imeripoti malori 69 ya bidhaa, ikijumlisha malori 39 ya mashirika yanayohudumia misaada ya kiutu ya UM katika Ghaza, yameruhusiwa kuingia kwenye eneo hilo kutokea Israel, kwa kupitia kivuko cha Kerem Shalom. Kadhalika UNSCO imearifu kwenye kivuko cha Rafah baina ya Misri na Ghaza, malori 15 yaliobeba chakula na madawa yaliruhusiwa kuingia Ghaza, na wagonjwa na majeruhi 18 walipelekwa Misri kwa matibabu kupitiai kituo hicho.

Baraza Kuu la UM Alkhamisi limeitisha kikao cha dharura, cha marudio, kusailia msiba wa vifo vinavyoendelea kuongezeka, na kuzingatia maafa yalioenea yenye kusumbua raia, kutokana na wiki tatu za mashambulio dhidi ya eneo liliokaliwa la WaFalastina la katika Tarafa ya Ghaza. Raisi wa Baraza Kuu, Miguel D’Escoto Brockmann kwenye taarifa yake mbele ya wajumbe wa kimataifa, alikumbusha kwamba licha ya kuwa Baraza la Usalama lilipitisha wiki iliopita azimio 1860 (2009), liliotoa mwito wa “kusimamisha mapigano haraka” kwenye Taarifa ya Ghaza, hata hivyo, “mashambulio hayo bado yaliendelezwa bila huruma .. wakati Ghaza ikiwaka moto.” Kikao hiki cha Baraza la Usalama kiliendelea kwa siku mbili mfululizo, na Ijumaa usiku kulipitishwa azimio liliotaka, kwa uzito mkuu “kuhishimu kikamilifu azimio 1860 (2009) la Baraza la Usalama, na kusimamisha haraka mapigano; na vile vile kuhakikisha kitendo hicho kitatekelezwa na kudumishwa, na kufuatiwa haraka na uhamishaji wa vikosi vya Israel kutoka Tarafa ya Ghaza.” Azimio vile vile limeshurutisha misaada ya kiutu kuingizwa katika Ghaza bila vizingiti, pamoja na kuruhusu vyakula, nishati na matibabu kuhudumiwa waathirika wote husika wa mapigano. Mataifa 142 yalipiga kura ya upendeleo, mataifa 4 yalitia kura ya upinzani na mataifa 8 kutopiga kura.