UNAMID inaahidi itaendelea kuhami raia Darfur Kusini, licha ya kufumka kwa mapigano
Minni Minawi, Ofisa Msaidizi wa Raisi na Kongozi wa jeshi la mgambo la Sudan la SLA/MM Ijumapili alizuru Makao Makuu ya Vikosi vya Amani vya Mchanganyiko vya UM/UA kwa Darfur (UNAMID) katika mji wa El Fasher na kukutana, kwa mashauriano, na Naibu Mjumbe Maalumu wa Pamoja wa UNAMID [Henry Anyidoho] na vile vile maofisa wa ngazi za juu wengine kuzingatia hali ya usalama katika mji wa Muhajeriya, Darfur Kusini .. ambapo katika siku za karibuni mapigano makali yalishuhudiwa huko baina ya kundi la JEM na SLA/MM.