Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msemaji wa UNRWA akiri hali shwari Ghaza lakini bado ni ya wasiwasi

Msemaji wa UNRWA akiri hali shwari Ghaza lakini bado ni ya wasiwasi

Chris Gunness, Msemaji wa Shirika la UM Linalofarajia Misaada ya Kihali kwa WaFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA) alihojiwa Ijumatatu, kwa kupitia njia ya simu, na Idhaa ya Redio ya UM-Geneva ambapo alielezea namna hali ilivyo sasa hivi katika Ghaza, baada ya kutangazwa vikosi vya Israel vinasimamisha mashambulizi:~

UM unatarajiwa kupeleka tume maalumu Ghaza kutathminia mahitaji hakika ya umma kufuatia ilani ya kusimamisha mapigano na mashambulizi. Kadhalika UM inahimiza wafadhili wakuu wa kimataifa kuharakisha mchango maridhawa wa dharura katika siku zijazo, ili kuiwezesha UM kuhudumia vyema wakazi waathirika katika Tarafa ya Ghaza.