Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kesi ya awali ya ICC inawashirikisha waathiriwa wa vita katika JKK

Kesi ya awali ya ICC inawashirikisha waathiriwa wa vita katika JKK

Ijumatatu kwenye mji wa Hague, Uholanzi Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) imeanza kusikiliza kesi ya Thomas Lubanga Dyilo, mtuhumiwa wa kwanza kukabidhiwa Mahakama tangu ilipoanza kazi zake. Kadhalika, kesi hii itawasilisha mara ya kwanza katika historia ya sheria ya kimataifa ambapo waathirika wa makosa ya jinai [ya vita] watashiriki kikamilifu kwenye kesi hiyo.