Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna wa Haki za Binadamu alaumu unyanyasaji unaopaliliwa na LRA katika JKK

Kamishna wa Haki za Binadamu alaumu unyanyasaji unaopaliliwa na LRA katika JKK

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, ameeleza kuwa ana wahka mkubwa juu ya ripoti alizopokea za kukithiri kwa vitendo vinavyokiuka na kutengua haki za binadamu, vinavyoendelezwa na wafuasi wa kundi la waasi wa Uganda wa LRA, katika kaskazini ya JKK.

“Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ameelezea khofu alionayo kuhusu kuendelea kwa vitendo vya unyanyasaji, na pia utenguzi wa haki za binadamu, vinavyoendelezwa na wafuasi wa kundi la waasi wa Uganda wa Lord Resistance Army (LRA) katika JKK; vile vile ana wahka juu ya operesheni za pamoja za kijeshi, zinazofanyika sasa hivi na vikosi vya Rwanda na JKK dhidi ya waasi wa kundi la FDLR, yaani lile kundi la wanajeshi wa mgambo wa KiHutu, waliokimbilia Kongo kufuatia mauaji ya kuangamiza [yaliotukia Rwanda] katika 1994, vitendo ambavyo anaamini vinahatarisha maisha ya raia, kwa ujumla. Kadhalika, Kamishna wa Haki za Binadamu ametoa mwito kwa makundi yote yaliojihusisha kwenye uhasama na mizozo kadha wa kadha iliopamba katika JKK, kujitahidi kuhishimu haki za binadamu, haraka, na kutekeleza sheria za kiutu za kimataifa, na pia kupendekeza jumuiya ya kimataifa itakapojaribu kusuluhisha mzozo wa mashariki, katika JKK, kwa njia ya amani, vile vile ihakikishe wale wote walioendeleza jinai ya vita watawajibika kufikishwa mahakamani na kukabili haki.”