28 Januari 2009
Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) leo mjini Geneva limewasilisha ripoti ya mwaka yenye kuashiria muongezeko mkubwa wa idadi ya watu wasiokuwa na kazi katika 2009, kwa sababu ya kuselelea, kwa nguvu, kwa mizozo ya kiuchumi ulimwenguni.