Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

KM ameripotiwa kukaribisha, kwa matumaini ya kutia moyo, uamuzi wa chama cha upinzani cha MDC kujiunga na serikali ya umoja wa taifa ya Zimbabwe, kama ilivyoidhinishwa kwenye Mapatano ya Amani ya 15 Septemba 2008 pamoja na mapendekezo ya Viongozi wa SADC ya 27 Januari 2009. UM imesema itafanya kila iwezalo na kuahidi mchango kamili utakaosaidia Mapatano ya 15 Septemba kutekelezwa nchini Zimbabwe kama inavyotakiwa. KM ameisihi Serikali ya Zimbabwe kuchukua kila hatua zinazohitajika kukabiliana na mizozo ya kiutu na kiuchumi ilioselelea nchini, na vile vile kuitaka ihishimu mifumo ya uhuru wa kidemokrasia katika nchi.

Shirika la UM Linalohudumia Wahamiaji (UNHCR) limeripoti wahamiaji 4,500 ziada kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati (JAK) karibuni waliwasili eneo la kusini-mashariki katika Chad, wakikwepa mashambulizi ya waasi waliofanya maskani katika JAK. Kufuatia tuko hili UM umetuma timu maalumu Chad kusini, karibu na mpaka na JAK, kutathminia mahitaji ya kiutu. Asilimia kubwa ya wahamiaji wa JAK walikuwa wanawake na watoto wadogo.

Kwenye ripoti mpya ya KM kuhusu majukumu ya kulinda na kuhifadhi raia, ilisisitizwa kwamba njia bora kabisa ya kukomesha uchafuzi wa maadili hayo ni kutayarisha miradi kamili ya UM, pamoja na mifumo maalumu yenye taratibu zitakazohakikisha dhamana ya kuhifadhi raia na umma hutekelezwa kidhati na Mataifa Wanachama.

Alkhamisi nchi tisa zilizowakilishwa kwenye mkutano wa kiwango cha juu, uliofanyika Djibouti na kuitishwa na Shirika la Kimtaifa juu ya Shughuli Bahari (IOM) zilitia sahihi Kanuni za Mwongozo kwenye juhudi zao za kupambana na uharamia wa vyombo vinavyosafiri kwenye eneo la Magharibi la Bahari ya Hindi na katika Ghuba ya Aden. Nchi hizo ni Djibouti, Ethiopia, Kenya, Bukini, Visiwa vya Maldives, Ushelsheli, Usomali, Tanzania na Yemen.

Msemaji wa KM ameripoti kuwa Ban Ki-moon anafuatilia kwa ukaribu sana hali katika Bukini baada ya kuzuka machafuko na vuurugu, hali iliosababisha darzeni za vifo katika mji wa Antananarivo. KM alinakiliwa akisema amchukizwa na kupotezwa maisha ya watu wasio hatia na ana wahka na usalama ulionyesha dalili za kuregarega. Aliitaka Serikali ya Bukini kuipa umbele kadhia ya kulinda umma, na kuyataka makundi yanayopingana kusuluhisha kutiofahamioana kwao kwa majadiliano yatakayojumlisha kila mtu na kwa utaratibu wa amani.

Ijumamosi ni siku ya mwisho kwa Ufaransa kuongoza shughuli za Baraza la Usalama kwa mwezi Januari. Kuanzia tarehe 01 Februari uraisi wa Baraza la Usalama utakabidhiwa Ujapani, cheo ambacho hudhaminiwa kwa duru wanachama wa taasisi hiyo ya kimataifa.