Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zimbabwe inasaidiwa na mashirika ya kimataifa kudhibiti miripuko ya kipindupindu

Zimbabwe inasaidiwa na mashirika ya kimataifa kudhibiti miripuko ya kipindupindu

UM umeripoti miripuko ya kipindupindu Zimbabwe ni hali inayohatarisha afya ya jamii kitaifa na hta katika mataifa jirani ya kusini mwa Afrika.

“Takwimu zilizokusanywa, hadi Disemba mosi, juu ya suala hili zinaonyesha watu 11,735 (elfu kumi na moja, mia saba nathelathini na tano) waliambukizwa na ugonjwa wa kipindupindu katika Zimbabwe; na kati ya idadi hiyo watu 484 (mia nne themanini na nne) walifariki. Uwiano wa vifo vya wagonjwa hawa ni kubwa sana, na imefika asilimia 04, na kwa hali kuzingatiwa kuwa imedhibitiwa, uwiano wa vifo hivi lazima uteremke chini ya asilimia moja! Kwa hivyo, hali katika Zimbabwe inamaanisha wagonjwa wingi wa kipindupindu hawapat matibabu ya kuridhisha, kwa wakati; na hata wakipatiwa huduma hizo humaanisha pia kuwa hawapewi matibabu mazuri na dawa hazitoshelezi tiba. Hivi sasa WHO inajihusisha na mashirika 10 mbalimbali, yanayojumlisha mashirika yasio ya kiserikali na mashirika ya UM, hali kadhalika, pamoja na Wizara ya Afya ya Zimbabwe, na wanajaribu kuendeleza juhudi za pamoja, za kuutekeleza mradi wa dharura wa WHO, wa kudhibiti janga la kipindupindu lenye kuathiri umma, takriban, katika majimbo yote nchini Zimbabwe, hususan katika mji mkuu wa Harare.”