Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO inasema mchango wa wakulima na wahudumia misitu unahitajika kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa

FAO inasema mchango wa wakulima na wahudumia misitu unahitajika kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti leo kwamba jamii za wakulima pamoja na ule umma unaotegemea riziki kutokana na shughuli za katika misitu, ni lazima jamii hizi, kuhusishwa kwenye huduma za kudhibiti uharibifu wa mazingira unaotokana na mabadiliko ya hali ya hewa, licha ya kuwa kadhia za kilimo na misitu ndio vyanzo vinavyochangisha katika uchochezi wa mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.